Kupitia kipidi cha RECAP & MANDO amezugumza namna wasanii Diamond Platnumz na Harmonize walivyorudisha tabasamu kwa wakongwe wa Bongo Fleva #ChidBenz na Professor jay tena kwenye muziki.
Siku za hivi karibuni tumeonna Hamonize ameweka wazi kuwa atakuwa na collabo tena na mongwe Professor Jay baada ya muda kupita lakini pia baada ya kupitia changamoto za kiafya kwa muda sasa.
Professor Jay tunajua ana collabo tayari na Harmonize inayoitwa YATAPITA lakini pia itafanyika nyingine, hivi ni kuendelea kumheshimisha Kaka yake Professor Jay ambaye ameweka alama kwenye muziki wa Bongo Fleva.
Lakini pia Diamond wakati wapo Mwanza kutambulisha wasanii wa Bongo Fleva alim-suprise Chid Benz kwa ngoma ya TUNAISHI NAO, hii sio collabo ya kwanza ya Diamond na Chid Benz maana tayari wana collabo mbili na hii ya tatu.
Collabo ya kwanza ni MPAKA KUCHEE ambapo Chid Benz alimshirikisha Diamond na AY lakini pia NALIA NA MENGI Diamond alimshirikisha Chid na hii BINADAMU (TUNAISHI NAO) Chid Benz ft Diamond inakuwa ya tatu.
Hii ni heshima kubwa sana kwa wakongwe hawa wa muziki wa Bongo Fleva.